Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Jawadi Amoli katika mazungumzo yake amezungumzia maana ya "mawaidha" na kusema:
Mawaidha, ambayo ni kazi ya malezi ya kiroho, ni tofauti na kufundisha. Mawaidha na malezi ni pale mtu anapo toa waadhi. Je! Ni nini maana ya kutoa waadhi? Kutoa waadhi ni kuwavuta watu kuielekea haki. Yaani mtu alete athari kwa msikilizaji kiasi cha kwamba amfanye yule msikilizaji aachane na dhambi. Mtu asipokuwa na nguvu ya mvuto, kama mfano wa sumaku, hotuba zake hazitakuwa na athari, mawaidha yake hayataathiri, na tabia zake pia hazitakuwa na athari yeyote.
Mawaidha ni kitu kinacho wavutia watu kuielekea haki, muda wa kuwa hatujakuwa kama sumaku, maneno yetu hayataweza kuleta athari katika jamii.
Maoni yako